12 Februari 2013 - 20:30

Jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran limetambulisha silaha yake mpya yenye uwezo wa kumshambulia yenyewe bila ya kuhitajia askari wa kuifyatua

Jenerali Aham Wahid ameeleza kuwa silaha hii inaitwa "Sair" 100 mm (automatic air defense gun)ni silaha ya kisasa yenye uwezo wa kumtafuta adui na kumshambulia yenyewe, silaha hii ina uwezo wa kupiga makombora 12 hadi 15 kwa dakika. ni muhimu kuashiria kuwa Jeshi la Iran limekuwa likisonga mbele katika nyanja tofauti za kiviwanda na kimaendeleo ikiwemo nyanja ya utengenezaji wa silaha mpya. haya yote ni matunda ya mapinduzi ya kiislamu.